Angalia Data za World Bank; Nani Zaidi - Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli Kwa Uchumi Tanzania
Labda hiyo graph haoinekani vizuri, lakini inachoonyesha ni kwamba kulingana na data za Benki ya dunia, tukitumia GDP per capital growth rate, katika kipindi cha Mwinyi, Mkapa na JK, Mkapa ndio aling'ara kwenye kuinua ukuzi wa uchumi, tunapolinganisha alipoingia na alipotoka, na kwa ujumla.
Japo kwa Mwinyi tunachoona ni miaka yake mitano ya mwisho - inaonyesha aliuacha uchumi katika hali mbaya kuliko kipindi chake cha kwanza cha miaka mitano. Mwinyi peke yake aliingiza Tanzania kwenye negative GDP per capital growth rate, hadi wastani wa -3%.
Mkapa alipochukua nchi aliuboresha uchumi zaidi sana ya Mwinyi alipouacha. Kuelekea mwishoni mwa kipindi cha Mkapa kasi ya ukuzi ilipungua, labda ni kipindi kila mtu alianza kuchukua chake! Kwa ujumla ukuzi wa uchumi wakati wa Mkapa ulikuwa na msimamo mzuri unaoeleweka, sio panda shuka ya Mwinyi na Kikwete.
Kikwete alipochukua toka kwa Mkapa ghafla uchumi alianza kuporoka chini zaidi ya pale alipouacha Mkapa. Jambo lililo wazi ni kwamba wakati wa Kikwete ukuzi wa uchumi ulikuwa hauna msimamo kamili, kila mwaka kupanda na kushuka kuonyesha Kikwete hakuwa na mwelekeo unaoeleweka katika mambo ya uchumi ukilinganisha na Mkapa. Kwa wastani Kikwete aliushusha uchumi kuliko alipouacha Mkapa.
Katika kipindi cha mwaka mmoja cha JPM, japo watu wanalalamika kwamba shilingi imeota miguu, lakini yeye amefikia rekodi ya GDP per capita growth rate ambayo haijawahi kufikiwa na maraisi wote waliomtangulia. Magufuli alipochukua tu nchi toka kwa Kiwete tulianza kupanda. Sasa hii inamaanisha nini kuelekea mbele tunasubiri kuona, na mwishoni mwa 2017 tutapata picha kamili.
Ila picha ya ujumla ni kwamba tangu 1990 hadi 2016 tumeenda vizuri sana. Katika kipindi cha Mwinyi na Kikwete kwa wastani hatukwenda mbele wala kurudi nyuma. Hadi sasa ni Mkapa peke yake aliyetuinua tangu mwaka 1990. Na Magufuli anaonekana ana mwelekeo wa kutuinua toka pale alipotuacha Mkapa.
NB. Data za 2016 kipindi cha JPM hapo juu ni halisi, isipokuwa zimefanywa wastani wa quarter tatu (January - September), Q1, Q2, Q3, badala ya nne za miaka mingine.
src "https://www.jamiiforums.com/attachments/upload_2017-1-27_14-59-25-png.464300/"
0 comments:
Post a Comment