Sunday, January 29, 2017

Treni mpya(Deluxe) yapata ajali Ruvu mkoani Pwani ikitokea Kigoma

Ajali hiyo imetokea maeneo ya Ruvu kwenda Ngeta(Kikongo), Kibaha mkoani Pwani. Ilikuwa inaelekea Dar. Ni ile Treni mpya (Deluxe) ========= Treni ya abiria ya Delux iliyokuwa ikitoka Kigoma kwenda Dar es Salaam imeanguka eneo la Ruvu mkoani Pwani.
Msemaji wa TRL, Medladjy Maez amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo aliyosema hali ni mbaya iliyotokea saa 9:40 alasiri.
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Boneventura Mushongi amesema ni kweli ajali na mabehewa manane yameanguka na watu watano wamejeruhiwa.
Treni mpya(Deluxe) yapata ajali Ruvu mkoani Pwani ikitokea Kigoma

0 comments:

Post a Comment