Ephraimu Mgawe na msaidizi wake, walifikishwa katika mahakamani wakikabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka kwa kusaini mkataba wa kuipa kazi kampuni ya ujenzi ya China communications Ltd bila kutangaza zabuni.
Msaidizi wa Mgawe ambaye walifikishwa wote mahakamani hapo ni naibu mkurugenzi mkuu PTA, Amadi Koshuma ambao wote walipandishwa kizimbani mbele ya hakimu mkazi mkuu, mfawidhi, Isaya Arufani katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es salaam.
Upande wa jamhuri uliongozwa na wakili wa serikali mkuu, Osward Tibabyekomya akisaidiana na mwendesha mashtaka wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU), Ben Linkolin.
Linkolin alidai kuwa Desemba 5, mwaka 2011 huko TPA, washtakiwa wakiwa waajiriwa wa mamlaka hiyo kwa nyadhifa hizo, walitumia vibaya madaraka yao.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa walitumia vibaya madaraka yao baada ya kusaini mkataba kati ya TPA na kampuni ya China communications na kuipa kazi ya ujenzi wa geti namba 13 na 14 ya mamlaka hiyo, bila kutangaza zabuni kinyume cha kifungu cha 31 cha sheria ya manunuzi namba 21 ya mwaka 2004.
0 comments:
Post a Comment