Saturday, February 4, 2017

Mwanamke wa Kitanzania akamatwa na Cocaine India

Thelma Mkandawire (38) raia wa Zambia and Pamela Devid Kiritta (41) raia wa Tanzania baada ya kukamatwa na kilo nne za cocaine leo nchini India.
Wanawake wawili wamekamatwa leo Jumamosi na kilo nne za cocaine nchini India. Wanawake hao wametajwa kama Pamela Devid Kiritta mwenye umri wa miaka 41 raia wa Tanzania na Thelma Mkandawire mwenye umri wa miaka 38 raia wa Zambia.
Wanawake hao wamekamatwa ndani ya hoteli moja iliyoko kusini mwa jiji la New Deilhi baada ya maafisa husika kutonywa kuwa walikuwa wanapeleka mzigo huo wa cocaine kwa mtu fulani. Mwanamke wa Zambia alisafiri na ndege ya kampuni moja ya Ulaya akitokea Addis Ababa. Maafisa hao walianza kumfuatilia mara tuu alipotua kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege wa IGI.
Baada ya kucheki out, Mzambia huyo alichukua teksi na kuondoka zake. Maafisa walimfuatilia mpaka kwenye hoteli moja iliyopo eneo la Mahipalpur ambapo partner wake Pamela alikuwa anasubiria mzigo. Wote wawili walikamatwa kabla ya kuondoka hotelini hapo. Ndani ya begi la Mzambia kulikuwa na mzigo wa kilo nne za cocaine ambazo zilikuwa zimefungwa kwa ustadi mkubwa sana kiasi kwamba machine za airport hazikuweza kugundua.
Alipohojiwa na maafisa hao, Pamela alisema alikuwa amepanga kwenye flat moja iliyoko Vasant Kunj tokea Januari 20 mwaka huu. Pamela amesema kuwa alikuwa anamfanyia kazi mwanaume mmoja wa Afrika ya Kusini. Pamela ameitembelea India mara tisa tokea mwaka 2006. Pia Pamela ameshatembelea nchini nyingine kama Ecuador, Afrika Ya Kusini na Kenya. Maafisa wa India wanahisi kuwa safari zake zinahusiana na biashara ya dawa za kulevya.
Kwa upande wa Mzambia (Thelma) alikamatwa Pakistani mwaka 2015 kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya. Pia ametemblea nchi za China na Hong Kong kwa biashara hiyo hiyo.
Chanzo: Two women from Africa held in Delhi for smuggling cocaine worth ₹30 crore =================== I wonder kama Pamela Devid Kiritta ana uhusijhano wowote na Lina Mkunde David Kiritta ambaye pia anajulikana kama Lenah Musyoka Mwenda.
Tarehe 10 February 2007, Lina Mkunde David Kiritta (Lenah Musyoka Mwenda) alikamatwa na kilo mbili za heroin katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Baada ya kukamatwa alishtakiwa na July 24, 2008 alikutwa na hatia ya kusafirisha heroin kinyume na sheria za Kenya. Kwa mshangao wa wengi, hakimu alimpa adhabu ya kifungo cha nje cha miaka 10 na haki ya kukata rufaa ndani ya siku 14.
DPP wa Kenya hakuridhishwa kabisa na hukumu ya hakimu na hivyo aliiomba Mahakama Kuu ifanye mapitio ya hukumu. Baada ya kupitia hukumu hiyo, Mahakama Kuu ya Kenya ilikubaliana na maombi ya DPP na kumtaka Lina Mkunde David Kiritta alias Lenah Musyoka Mwende alipe faini ya shilingi milioni 6 za Kenya au aende jela miaka 8. Pamoja na adhabu hiyo, Mahakama Kuu iliamuru pia aende jela miaka mitatu na nusu kuanzia siku aliyokamatwa.
Hukumu ya Mahakama Kuu inapatika hapa: Criminal Revision Case 62 of 2008 - Kenya Law

0 comments:

Post a Comment