Monday, February 6, 2017

Dawa za Kulevya: Wema adai Makonda anatembea na Agnes Masogange ndio maana hakamatwi

Sakata la Madawa ya Kulevya limechukua sura mpya kufuatia mwanadada mashuhuri Wema Sepetu, ambaye ni mmoja wa watuhumiwa, kutoa ya moyoni juu ya sakata zima la kukamatwa kwao na kuhusisha tukio hilo na hila dhidi yake.
Pamoja na mambo mengine, Wema amedai kwamba RC Paul Makonda anatembea na Agnes Masogange na amempangia nyumba Makongo ndio maana hajakamatwa ktk kadhia ya Dawa za Kulevya.
Operesheni ya kukamata wanaojihusisha na madawa ya kulevya ilianzishwa na Paul Makonda mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo alitaja majina ya watu mbalimbali wanaohitajika kituoni kwa ajili ya mahojiano, wakiwemo wasanii na maaskari polisi.
===== Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda Simon Sirro amesema kuwa mpaka sasa Jeshi la Polisi linawashikilia watuhumiwa wa Dawa za Kulevya 112 na jumla ya kete 299 huku 12 kati yao wakifikishwa Mahakamani.
Kwa taarifa hii soma > Makonda: Watuhumiwa madawa ya kulevya kuanza kupandishwa kizimbani leo au kesho

0 comments:

Post a Comment