Monday, February 6, 2017

Rais Magufuli apigilia msumari jeneza la wauza Dawa za Kulevya, asema si kazi ya Makonda pekee

Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaohusika na Dawa za Kulevya. Asema si kazi ya Makonda pekee. Rais Magufulia amesema hakuna wa kuachwa hata akiwa mkewe Mama Janet Magufuli, na kuongeza kuwa wakamatwe bila ya kujali majina yao. Rais Magufuli amesema anamuomba Jaji Mkuu asizicheleweshe kesi za madawa ya kulevya kwani kuna mtuhumiwa mkubwa wa Dawa za Kulevya anashikiliwa Lindi bila ya kufikishwa Mahakamani. Najua IGP Mangu watu walikupigia simu wanakupa ushauri kuhusu Dawa za Kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa IGP. Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni.

0 comments:

Post a Comment