Friday, February 3, 2017

Yabainika: Mjane wa Tanga aliyemlilia Rais Magufuli si tapeli. Nyaraka nyeti zaibuliwa MJANE kutoka Tanga, Swabaha Mohamed Shosi aliyewashtaki baadhi ya watendaji wa Serikali kwa Rais John Magufuli hapo jana akidai kuzungushwa kupewa haki yake ya mirathi si tapeli kama inavyosambazwa mitandaoni, FikraPevu imejiridhisha. FikraPevu ililazimika kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba ili kupata ukweli wa tuhuma zilizokuwa zikielekezwa kwa mama huyo mitandaoni na aliithibitishia kuwa Jeshi lake halijawahi kupokea malalamiko yoyote dhidi ya mjane huyo kuhusika na utapeli. Zimekuwepo jitihada za makusudi mitandaoni zikitoa taarifa zinazoonyesha kuwa kuna watu wanamfahamu kwa undani mjane huyo na kudai ni tapeli aliyekubuhu, bila kuwataja waliowahi kutapeliwa, walitapeliwa nini na lini walifanyiwa utapeli huo. TUNACHOKIFAHAMU: FikraPevu imepata kuziona nyaraka mbalimbali zinazohusiana na sakata la mjane huyu ikiwemo barua toka kwa Wakala wa Usajili na Ufilisi (RITA) ya tarehe 13 Februari 2014 kwenda kwa Mkuu wa Upelelezi kuwa nyaraka za ndoa ya mama huyo ni halali.

0 comments:

Post a Comment